KUNGURU; A Swahili Poem by Robinson Mbigili

Posted by

image

KUNGURU

Salamu ya kunguru si doa kwenye kaniki ,
ni kukukumbusha umuhimu wa manati,
Harakati chafu ya nchi kua jalala,
wakubwa mmekanyaga chechele,
Ujinga ni fani ya mdhalimu,sauti hii haki wataona makelele
Neno uchafu linauchungu,na kwangu ni kadhalika,
Wakubwa Kuwatusi sipendi,nanyi sizani kama mwataka,
Tunzi katika utunzaji,wakubwa mmekuwa wababaishaji,
Mazingira yetu shokomzoba,kama safari viuno vinaitaji tiba,
Kuhifadhi kidogo kilichopo ni ushujaa
pasipo angaza udogo wa mshumaa utafaa,
Somo gumu kwa mwanafunzi ni kumulewa mwalimu,
kukumbatia uchafu ni mapenzi ya mwendawazimu,
Ni salamu ya kunguru tu,si doa si dosari ,wakubwa kunguru naruka nimeianza safari.

Wakubwa mjomba aliwaita ,njooni endeleeni kuja mtayaona mliyoyaacha
Mkianza kuja msiyaruke yaliyotuama maana ndo tunayokunywa ,
Ule wimbo wenu wa mbele kwa mbele ni mzuri japo mngeongeza na mlio wa kinanda ,,
Hili la mazingira  haliitaji kijani kijani  ,wala magwanda
Pengine mngetuonea huruma kwa lile jua la jangwani,bila mifereji huku kwetu taabani,
Alipokuja njiwa ,hadi za huku kwetu zilipigwa deki, ni sauti ya kunguru tu labda ndo maana hamnikumbuki.
Amakweli kipofu haitaji miwani wala tochi gizani,mdogo mdogo mikono na kelele za ndio mezani,
Maisha yetu nzi wakwetu kipindupindi mshkaji wetu ,wakubwa kumbukeni mpishi hadhuriki na chumvi,na nyoka kamwe haruki viunzi,najua mtazifata tena,

By; Robinson mbigili
0659559298

YOURS FOR FREE! MY FIVE-STAR BOOK "FIRE UP YOUR WRITING SERIES"
I agree to have my personal information transfered to MailChimp ( more information )
The Twelve (12) Small Potent Episodes Any Writer Can Practice & Learn From. GRAB YOUR FREE COPY NOW... Did I say for free?
I hate spam. I will not share your email address with anyone. PINKY SWEAR..
Julius Kessy
Follow me

Julius Kessy

Founding Writer, and CEO at My Writers Bureau
Howdy friend! I'm Julius, a quite, a bit shy, but easy going guy... Thanks for stopping by! At My Writers Bureau, I write for my readers and clients, meanwhile honing my writing skills. I like writing sentences that match out, one after another, polished and crisp, like soldiers on a parade ground! And I can help you do the same. Starting this blog, just out of a hobby, and seeing it growing pretty fast, is a joy! Help me to spread the word.
Julius Kessy
Follow me