FUNGU LETU FUNGU; A Swahili Poem by Robinson Mbigili

Posted by

image

FUNGU LETU FUNGU

Kujifunza baada ya kufeli ,si somo jipyaa
Tusijecheka chongo na hali zetu tumefunika,
Utamaduni adhim   na bangili ?
Asali na maziwa chini ya ulimi ndo utamu wa Kiswahili,
Watanzania tumeitupa tunu 
Tumeitawanya asili na kujigawa kwa mafungu,
Fungu letu fungu, hili lapilli kaleta mzungu

Huyu kipuli na mlegezo ulioacha nchi wazi,
Uchafu wa giza nyuma ya kivuli cha utandawazi
Mmelipendea nini gitaa mkalitupa zeze na zumari?
Ngozi mmeifanya ramani ngoma zetu mmezitia misumari,
Utumwa ni kukosa fursa ya kujituma
Jeuri ya shingo bila jicho ni kugeuka pasi kuona nyuma
Tafakari ya weusi haiishii kwenye ngozi, lahaasha huuifata tamaduni
Mama Tanzania hili la ushoga ni jipu uchungu
Mjomba fungu letu fungu , hili la tatu pia kaleta mzungu.

Sikuzote mwenda usiku amesifiwa kulipokucha,
Utupu nao ufahari  mama na mwana hakuna tofauti
Udaku na kusagana ndo mzigo uliokuja kwa ndege na boti
Mganga hana ombi nduguu,hilo ni shartii
Hata kichogo hufaa ngata ya duara
Kuhusu vikuku natania tu ndugu ni masiharaa,
Sifa ya uozo ni kunuka,ngono na ushoga vinafuka.

Tujisifu kwa lipi kama mnaimba kwa lugha ya kamusi?
Mmeyajaza yakwao na chachu ya matusi
Amakweli alielala na mgonjwa ndo anajua maugulio,
Tumeikimbilia chai,tukapewa majani kwenye chujio,
Viatu tulivyovaa havitutoshi ,jamaa hawakutupima miguu,
Tafakari ya hili ni ujinga wa bei nafuu,
Kweli fungu letu lilikuwa fungu ,hili  la mwisho pia kaleta mzungu.

Wapendwa nia yangu si kuwarudisha nyuma,
Lahaasha kuwatoa kwenye fungu la utumwa,
Gari la kuvutwa haliovateki ndugu
heri kukata kamba tukimbie na kokoteni letu
Fungu lao ni la kwao ,linatosha kwa mboga yao tu,
Kwa kujifanya tunathamini ,tunacheza ngoma uwanja wa ndege
Huu ni unafiki uliokithiri muda,
Pengine tujifunze kuwa na kibuli chenye faida.
Wapendwa fungu ni fungu letu katupa mungu
Fungu lao fungu ,….huu ujinga katuletea mzungu.

By; Robinson Mbigili
      0659 559 298

YOURS FOR FREE! MY FIVE-STAR BOOK "FIRE UP YOUR WRITING SERIES"
I agree to have my personal information transfered to MailChimp ( more information )
The Twelve (12) Small Potent Episodes Any Writer Can Practice & Learn From. GRAB YOUR FREE COPY NOW... Did I say for free?
I hate spam. I will not share your email address with anyone. PINKY SWEAR..
Julius Kessy
Follow me

Julius Kessy

Founding Writer, and CEO at My Writers Bureau
Howdy friend! I'm Julius, a quite, a bit shy, but easy going guy... Thanks for stopping by! At My Writers Bureau, I write for my readers and clients, meanwhile honing my writing skills. I can help you do the same. Starting this blog, just out of a hobby, and seeing it growing pretty fast, is a joy! Feel free to leave your comment and help me spread the word.
Julius Kessy
Follow me