NYUMA YANGU-RIWAYA YA KIJANA MTANZANIA

Posted by
Reading Time: 2 minutes

image

Nyuma Yangu ni riwaya inayoangazia namna jamii inavyoweza kuathiri maisha pale unapokosekana ukweli wa jambo ikiwa mtuumiwa ndio mwenye ukweli wa hilo jambo.Nyuma yangu inamchukua Mwanamke na kumpitisha katika mazingira yake na kuonyesha changamoto anazokumbana nazo ikufikia malengo.
Pia Nyuma Yangu inaichora familia na kuangalia malezi ndani ya familia na maamuzi ya wazazi juu ya utendaji wa watoto.Familia ndio msingi na mchoro wa mtoto.Chochote kitakacho onekana machoni kwa mtoto kinaakisi familia yake.
Marafiki ni zawadi toka kwa Mungu,Nyuma yangu inaenda mbali kumbeba rafiki na kuonyesha namna marafiki wanavyoweza kufifisha ndoto zetu katika maisha.Hatuwezi kukwepa kuwa na marafiki lakini lazima tupime nafasi ya rafiki katika maisha yako.Mkiwa wawili jua kuwa mnawaza tofauti hata kama mtakubaliana kwenye mambo fulani jua hamtaweza kuwaza ivyo kwa wakati wote.
Tamaa,pale unafikiria kufanya au kupata zaidi ya uwezo wako kumbuka unaweza kujikuta unaumiza watu wengine.”Kila mtu atakula kulingana na urefu wa kamba yake.”Hadithi ya Nyuma yangu inajenga umbo la namna tamaa inavyoweza kufifisha uwezo wa kufikiri vyema  juu ya wengine na thamani yao katika dunia.
Riwaya ya Nyuma Yangu imejengwa katika mandhari ya kitanzania ikichukua uhalisia wa maisha ya Afrika.Nyumba yangu inaitaji kujenga jamii mpya yenye kuthamini nafasi ya wengine katika kufanya maamuzi na kusikilizwa.Hukumu zetu ziwe kinyume cha hisia zetu zaidi tuangalie mazingira na namna mtu anavyojaribu kutoa maelezo juu ya matokeo ya utendaji wake.
Nyuma yangu ni riwaya yangu ya kwanza kukiwa na nyingi zinakuja kuijenga jamii yenye kuheshimu thamani yake na kuilinda.Jamii itayokuwa na matokeo bora kwa taifa na dunia huku ikiweka vipaumbele vya utu wema na huruma kwa wengine.
#Ansgar Haule/Social activist/Story Writer
#Contact:0756002661,H.ansgar@yahoo.com

TUNALENGA KUNYANYUA VIJANA WAANDISHI TOKA WALIPO KUFIKIA MALENGO YAO.

YOURS FOR FREE! MY FIVE-STAR BOOK "FIRE UP YOUR WRITING SERIES"
I agree to have my personal information transfered to MailChimp ( more information )
The Twelve (12) Small Potent Episodes Any Writer Can Practice & Learn From. GRAB YOUR FREE COPY NOW... Did I say for free?
I hate spam. I will not share your email address with anyone. PINKY SWEAR..
Julius Kessy
Follow me

Julius Kessy

Owner & CEO at My Writers Bureau
Hi there... Welcome to My Writers Bureau. I'm a freelance writer, English to Swahili translator, and a virtual assistant. The journey of working online hasn't been easy but I enjoy every bit of it. This is my side hustle business apart from my full-time job. I can help you also start an online empire and create your own economy. Hang in there!
Julius Kessy
Follow me

Comments are closed.