BONGO STYLE USHINDANI

Posted by
Reading Time: 3 minutes

Bongo Style Competition inalenga kutambua, kutoa tuzo/zawadi na kusapoti wabunifu mitindo vijana na wapiga picha vijana na kuhamasisha vijana kupenda sanaa na tamaduni zao. Bongo Style Competition kwa wabunifu mitindo vijana na wapiga picha vijana ni kwa ajili ya vijana wenye umri wa miaka kati ya 18 hadi 25. Shindano lina vipengere viwili: Mbunifu Mitindo bora kijana na Mpiga picha bora kijana.

Vigezo na Masharti

Shindano ni kwa vijana wa kitanzania tu wenye umri wa miaka kati ya 18 hadi 25). Vigezo na masharti yafuatayo yatazingatiwa wakati wa tathmini:

Ubunifu, kujieleza, upekee na usafi wa kazi/muonekano wa kazi.
Kazi zote ziongelee tamaduni za kitanzania, urithi/amali na hali halisi ya kitanzania. Iwe inayoweza kuchapishwa (isiwe inayokiuka maadili, isiwe na udhalilishaji wa aina yoyote) na isiwe imewahi kuchapishwa/kutolewa au kushindanishwa kwenye mashindano mengine kabla.
kazi iwe ni ya ubunifu wa mshiriki kwa asilimia 100%.
KUMBUKA: Vigezo na masharti mengine yapo kwenye maelezo ya kila kipengere cha ushindani. 

Vipengere vya Ushindani

Mbunifu Mitindo Kijana

Kipengere hiki kinalenga kutafuta vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 25 wenye mapenzi katika ubunifu mitindo, kipengere hiki kinalenga kuwasaidia wabunifu mitindo vijana kuona fursa mbalimbali zilizoko mbele yao. Washiriki katika kipengere hiki wanatakiwa

»kuwa raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 25 wakati wa kujiandikisha kushiriki shindano
»mwenye mapenzi ya dhati ya kuwa mbunifu mitindo
»atatakiwa atume picha mnato au video au vyote (jumla tatu) zinazoonyesha kazi zake za kibunifu
»Ubunifu huo ni lazima uwakilishe utamaduni wa kitanzania

Jiandikishe hapa !
FOMU YA KUJIANDIKISHA

Je umekwisha jiandikisha? Sasa unaweza kutuma kazi yako !

FOMU YA KUTUMA KAZI

Mpiga picha kijana

Ni ukweli usiopingika kuwa Nyanja ya upigaji picha kama ilivyo Nyanja ya mitindo inakuwa kwa kasi ya kufurahisha; na kusababisha hitaji kubwa la wapiga picha wa kitaalamu na wenye mapenzi na kazi hii. kipengere hiki kinalenga kutafuta vijana kama hawa.  Washiriki katika kipengere hiki wanatakiwa

»kuwa raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 25 wakati wa kujiandikisha kushiriki shindano.
»Mwenye mapenzi ya dhati ya kuwa mpiga picha
»Anatakiwa kutuma picha zake tatu hadi tano (zinaweza kuwa ni picha za habari/kiuandishi, au zinaonyesha sanaa za kitanzania au za kitamaduni au mchanganyiko wa vyote)
»ukubwa wa Picha usizidi MB tatu na usipungue MB mbili
»iwe ni picha inayojieleza
»kila picha ni lazima iwe na kichwa cha habari na maelezo.

Jiandikishe hapa !

FOMU YA KUJIANDIKISHA

Je umekwisha jiandikisha? Sasa unaweza kutuma kazi yako !

FOMU YA KUTUMA KAZI

Muongozo

Jinsi/namna ya kushiriki:
»Jiandikishe(fomu ya kujiandikisha)
»tengeneza kazi yako
»Itume kazi yako (fomu ya kutuma kazi)
»kila kazi lazima iwe na kichwa cha habari.
»ushiriki wote lazima uzingatie uelewa wa taarifa za vigezo na masharti ya shindano.

Tarehe za Mwisho wa Kushiriki

»Tarehe 11 mwezi wa kumi: Mwisho wa kujiandikisha kwenye mtandao
»Tarehe 15 mwezi wa kumi: mwisho wa kutuma kazi
»Tarehe 20 mwezi wa kumi : Kutangaza 20 bora
»Tarehe 4-5 mwezi wa kumi na moja (Mafunzo kwa washiriki 20 bora)
»Tarehe 8 mwezi wa kumi na moja – kutangaza kumi bora kwa ajili ya fainali
»Tarehe 9 hadi 22 mwezi wa kumi na moja: Upigaji kura kwenye mtandao
»Tarehe 27 mwezi wa kumi na moja: Kutangaza washindi

Zawadi

mshindi wa kila kipengere (Mbunifu mitindo na mpiga picha) atajishindia Tsh milioni moja pesa taslimu na safari ya ubelgiji kuonyesha kazi zao). Safari inatarajiwa kuwa mwezi wa tatu mwaka 2016. Washiriki wote waliongia fainali watapatiwa misaada mbalimbali katika kuendeleza vipaji vyao. Msaada huu utakuwa katika kuwatangaza, kuwakuza, na kusaidia umiliki wa kazi zao kisheria.

image

Unaweza jiunganisha nami kupitia
Facebook,Instagram,Google+ na LinkedIn kwa kutumia jina; Julius P. Kessy

Unaweza nifuata Twitter
Kwa kutumia @PK_julius

YOURS FOR FREE! MY FIVE-STAR BOOK "FIRE UP YOUR WRITING SERIES"
I agree to have my personal information transfered to MailChimp ( more information )
The Twelve (12) Small Potent Episodes Any Writer Can Practice & Learn From. GRAB YOUR FREE COPY NOW... Did I say for free?
I hate spam. I will not share your email address with anyone. PINKY SWEAR..
Julius Kessy
Follow me

Julius Kessy

Owner & CEO at My Writers Bureau
Hi there... Welcome to My Writers Bureau. I'm a freelance writer, English to Swahili translator, and a virtual assistant. The journey of working online hasn't been easy but I enjoy every bit of it. This is my side hustle business apart from my full-time job. I can help you also start an online empire and create your own economy. Hang in there!
Julius Kessy
Follow me